HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Tuesday, December 9, 2008

HISTORIA YA JOMO KENYATTA




KABURI LA JOMO KENYATTA LILILOJENGWA KATIKA ENEO LA BUNGE



BENDERA YA KENYA


Jomo Kenyatta (1893-1978) alikuwa ni Rais wa kwanza wa Kenya,alizaliwa mwaka 1893 jina lake halisi ni Johnstone Kamau wa Ngengi. Alipewa jina la utani ambalo ni mkuki wa Moto (Burning Spear). Jina la Kenyata lilitokana na Mkanda aliopenda kuuvaa ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wagikuyu wanauita Kenyata. Kabila lake lilikuwa ni Mgikuyu. Alisoma katika shule ya Kanisa la Wamisheni wa Kiskoti.

Baada ya kuhitimu aliajiriwa kama karani na msoma mita wa manispaa ya Nairobi, alioa mke wake wa kwanza ambaye ni Grace Wahu.

Azma yake ya kutaka kuikomboa ardhi ya Wagikuyu ilimfanya kuweza kuwaunganisha Wagikuyu naye,akawa katibu wao mwaka 1928. Mwaka 1930 alitembelea Marekani na Uingereza ambako aliishi miaka 15 na kufanikiwa kumuoa mwalimu wa kiingereza ambaye aliitwa Edna Kenyata. Alirudi Kenya mwaka 1946 na alichaguliwa kuwa rais wa chama cha siasa cha Kenya African Union (KANU). Alihamasisha kukomesha ubaguzi wa rangi,kuwa na mwamko wa kisiasa,pamoja na mambo mengine yanayompa mwafrika heshima na Utu.

Aliandika kitabu kiitwacho Facing Mount Kenya kilichohusu ukombozi na historia ya Wagikuyu. Alikuwa pia ni mhariri na mwanzilishi wa gazeti la kwanza kwa lugha ya Gikuyu ambalo liliitwa Muiguitaani.

Kutokana na kuhusishwa na harakati za vita vya msituni vya kundi la MAUMAU, alihukumiwa miaka 7 jela mwaka 1952. Huwezi kuzungumza historia ya Kenyatta bila ya kutaja MAUMAU.

Baadaye alioa mke mwingine wa 3 ambaye aliitwa mama Ngina Kenyatta ambaye alikuja kuwa mke wa rais wa kwanza ambaye ndiye mama yake na Uhuru Kenyatta.

Juni 1 1963 Kenya ilipata madaraka na Jomo Kenyatta alitawazwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kenya.

Kenyatta alifariki mjini Mombasa tarehe 18 Agosti 1978 na kuzikwa jijini Nairobi kwenye jengo la Bunge

No comments: