HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Sunday, December 14, 2008

JE UNAJUA HISTORIA YA MAPIRAMIDI YALIYOPO HUKO MISRI

HAYA NDIYO MAPIRAMIDI YA GIZA,LA UPANDE WA KUSHOTO LINAITWA MYKERINOS, KATIKATI KHEFREN NA KULIA NI CHEOPS

Piramidi za giza ni kati ya majengo yanayojukana zaidi duniani,Yapo kando kando ya bonde la mto Nile karibu na mji wa Giza,takribani kilometa 15 kutoka Kairo katika Misri.

Piramidi hizi ni mabaki ya eneo kubwa la makaburi ya enzi za Misri ya Kale.Wafalme na maafisa wa juu walizikwa hapa.

Mapiramidi 3 makubwa yamepewa majina kufuatana na mafarao au Wafalme wa Misri waliozikwa ndani yao,Mapiramidi hayo ni Cheops, Khefren na Mykerinons

Uti wa mgongo wa nchi ya Misri ulikuwa ni mto nile. Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa lakini umwagiliaji wa mashamba kwa njia ya maji ya mto,utaratibu ambao ulileta mazao mazuri yaliolisha watu wengi. Mahitaji ya kupanga na kutunza mifereji pamoja na mitambo ya umwagiliaji,na kusimamia ugawaji wa maji yaliyosababisha kutokea kwa vyanzo vya Hisabati na Mwandiko. Mwandiko wa Misri ulikuwa hiroglifi ulikuwa ni mwandiko uliokuwa kwenye mfumo wa picha

No comments: