HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Tuesday, December 9, 2008

MFAHAMU PAPA BENEDICTO XVI





Papa Benedicto XVI alizaliwa tarehe 16 Aprili 1927 , jina lake la kuzaliwa alikuwa akiitwa Joseph Alois Ratzinger,ni papa tangu tarehe 19 Aprili 2005 baada ya kifo cha Yohana paulo II.

Ni mwandamizi wa 264 wa Mtume Petro na Papa wa kwanza kutoka Ujerumani baada ya miaka 1000 hivi.

Alipadirishwa tarehe 29 Juni 1951 pamoja na kaka yake Georg

Baada ya kupata udaktari katika teolojia na kufundisha miaka kadhaa, alishiriki kama mtaalamu katika Mtaguso Mkuu wa Vatikano II

Tarehe 24 Machi 1977 alichaguliwa na papa Paulo VI kuwa Askofu mkuu wa Munchen na Frisingen akapewa daraja hiyo tarehe 28 Mei mwaka 1977.

Tarehe 27 Juni 1977 Paulo VI alimteua pia kuwa Kardinali na kutokana na cheo hicho alishiriki uchaguzi wa Papa Yohane Paulo I na Yohane Paulo II mwaka 1978.

Tarehe 25 Novemba 1981 Yohane Paulo II alimteua kuwa mkuu wa Idara ya Mafundisho ya Imani. Hivyo tarehe 15 Februari 1982 aliacha uongozi wa jimbo kuu akashika kazi hiyo mpya mpaka alipochaguliwa kuwa papa

No comments: