HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Wednesday, August 6, 2008

PANYA WAHITIMU CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE






Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika,Dk Mathayo David Mathayo amesema panya 30 wamefuzu katika Chuo kikuu cha kilimo cha SUA yanayowawezesha kugundua eneo lililo na mabomu yaliyotegwa ardhini.

Naibu waziri huyo amesema hayo katika ukumbi wa Bunge,kuwa kuna panya wengine 50 ambao wapo katika hatua mbali mbali za utafiti huo unaofanywa kwa ushirikiano na nchi za Ubelgiji na Msumbiji.

'' ... Hadi sasa panya 18 wamepelekwa Msumbiji kwa shughuli za kuvumbua maeneo yaliyotegwa mabomu ardhini,na hakuna nchi yoyote iliyoomba utaalamu huo ... '' Alisema Dk Mathayo na kusisitiza panya hao hawauzwi.

Naibu Waziri huyo alisema panya hao hawauzwi kwasababu lengo la utafiti huo ni kuhudumia jamii kuondokana na adha ya mabomu ya kutegwa ardhini,na sio kwa lengo la biashara.

Dk Mathayo alisema kuna aina 25 za panya waharibifu wa mazao hapa nchini,na kwa zaidi ya miaka 10 sasa panya wa aina 3 hususani panya pori,panya dari na panya majani,wamekuwa wakisababisha uharibifu mkubwa wa mazao.

Alisema wanapotokea katika milipuko ya uharibifu,Serikali huingilia kati na kuwadhibiti.Lakini panya wanaofundishwa katika Chuo kikuu cha Sokoine ni panya buku ambao hawajafikia katika hatua ya mlipuko na hivyo hawasababishi uharibifu mkubwa wa mazao

'' ... Aidha Wizara inapenda kutoa ufafanuzi kuwa panya hao wanafundishwa kuvumbua maeneo yaliyotegwa mabomu ardhini kwa kunusa baruti,na mara baada ya panya hao kuvumbua eneo lililotengwa bomu,Wataalamu huyategua ... '' . Alisema Dk Mathayo

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Professa Peter Msola akizungumza swala la tuzo kwa wataalam wa SUA wanaoendesha utafiti huo,alisema Serikali inatambua kazi ya utafiti wao kuwa ni nzuri.

Alisema kwa kuwa vyuo vikuu vina kazi ya kufundisha,kutoa ushauri na kufanya utafiti.Hivyo basi kufuatia taratibu za vyuo,tuzo hutolewa ikiwa ni pamoja na kupandishwa vyeo,jambo ambalo haliwezi kufanywa kwa wataalam isipokuwa mpaka wafanye tafiti.

Awali Haroud Said Masoud ( CCM ),alitaka kujua ikiwa imedhibitishwa kuwa wataalam wa chuo kikuu cha Sokoine wanatoa taaluma kwa panya kuweza kutegua mabomu,na kwamba panya hao wakitoweka kabisa itakuaje kwa nchi yetu?.

Mbunge Huyo alitaka kujua iwapo utafiti huo ni wa kweli,na ni panya wangapi wameshapewa taaluma hiyo,pia alitaka kujua kama kuna nchi yoyote imeomba kupewa panya hao na taaluma ya kugundua mabomu kutoka Tanzania.Mbunge huyo alitaka kujua ni fedha kiasi gani zinazotozwa kwa panya mmoja aliyechukuliwa nje kufanya kazi hiyo.


( Rafiki yangu uliyesoma ukurasa huu,nimeona nikuandikie ili ujue ni jinsi gani ulivyo wa pekee.Inawezekana umeshawahi kudharauliwa kuwa huwezi kufanya hiki au kile,au kwasababu tu uliwahi kupata matokeo mabaya ulipokuwa shuleni,basi ukajidharau na watu walipokucheka ndio kabisa ukazidi kukata tamaa na kujiona wewe si kitu.Rafiki wewe una akili kuliko kiumbe kingine chochote hapa Duniani matokeo ya shuleni yasikufanye upate vidonda vya tumbo,wewe ni wa pekee na nakwambia una kitu ndani yako ambacho MUNGU amekuumba nacho cha pekee ili kubadilisha maisha yako,hicho kitu hakuna mtu mwingine alichonacho ila ni wewe tu,hicho kitu ni KIPAJI.Usinishangae ninamaanisha una kipaji cha kipekee ambacho ukikigundua na kupata ELIMU YAKE SAHIHI YA KIPAJI CHAKE,HALAFU UKAFANYA UTAFITI WA SOKO LA KIPAJI CHAKO LIPO WAPI,KISHA UKAJITUMA KUFANYIA KAZI KIPAJI CHAKO.Nakwambia watu wale wale waliokudharau wataabika na kukuheshimu.Hebu tazama panya buku,watafiti baada ya kugundua kuwa hawa wadudu ni noma kwa kunusa,wakawafundisha kunusa baruti,wakiwa na maana panya wakiizoea toka utoto kunusa baruti basi wakikuwa wataweza kugundua bomu lililochimbiwa,maana aina yoyote ya bomu ni lazima liwe na baruti ndani yake (hapo waliwapa elimu sahihi juu ya kipaji chao),Kisha hawakuishia hapo wakatafuta soko lao,wakapata Msumbiji,wadudu wakapanda ndege na kujituma kufanya kazi.Najua sasa una maswali moyoni mwako,ukiniuliza Zablon mbona mimi nipo nipo tu na sielewi kipaji changu?.Mimi nakujibu unacho,cha kufanya anza kujichunguza unapendelea kufanya nini mara kwa mara,nikimaanisha jambo unalopendelea kufanya mara nyingi kwa moyo wa kupenda,au ukimwangalia mtu akifanya jambo hilo unatamani kumwangalia basi hiyo ni dalili.Lakini Tafadhali usikurupuke tafuta njia kuhakikisha kuwa ni kweli?)

No comments: