Mathalani kama tabia yako inakuzuia kupanda cheo kazini,au inakufanya ukose mafanikio katika maisha,au ukosane na watu au kugombanisha watu ,au uvunje uhusiano na watu,au inakukosesha fursa ya kufurahi,au inakufanya uingie gharama,ni wazi kuwa unapaswa kuiacha.
Kama unadhani hauna tabia inayokusumbua kwa namna moja wapo kati ya hizo nilizokutajia,uliza watu wanaokuzunguka.Na kama utabaini tabia hiyo haiashirii wema kwa mustabali wa maisha yako,utapaswa kuchukua hatua muhimu ili kuivunja.
HATUA ZA KUFUATA KUACHA TABIA ULIYOIZOEA
- KIRI KWAMBA UNAYO TABIA ISIYOFAA
Tabia ni kitu kinachojirudia mara kwa mara na pengine mtu mwenye tabia fulani hupata manufaa fulani na kama si ya mali basi ni ya kisaikolojia,vinginevyo angeacha.Lakini tabia ni sehemu ya maisha ya mtu ambayo imeachwa bila udhibiti wowote wa mhusika.
Ukishatambua na kukiri tatizo lako,angalia undani wake na kubaini matatizo unayoweza kuwa unasababisha kutokana na tabia hiyo.Ukweli huo utakusaidia unapoanza mchakato wa kuacha tabia hiyo.
- FANYA TAFAKURI YAKINIFU
Baadhi ya tabia huwa hazitokani na tafakuri za mtu.Mtu anaweza kulalamika au kusema uongo,au kusengenya bila kuwa na nia ya dhati ya kufanya hivyo,lakini akawa amewakwaza watu au kukwaza maendeleo yake mwenyewe.
Dawa ya tatizo hili haliji mara moja,bali mara kwa mara unapojikuta ukifanya jambo ambalo si la haki,mathalani unapojikuta ukimsema mtu vibaya ,shtuka na kujiuliza kama kweli unalolifanya ni la haki .Jiulize pia kama ukimkuta mtu akikusengenya ungejisikia vipi au ungemuanaje?.
Ukifanya tafakari ya aina hii,jiwekee msimamo kuwa hutaendelea na hicho unachokifanya.
- HEPUKA MAZINGIRA YANAYOKUPONZA
Mazingira na muktadha huathiri mwenendo wa mtu.Ukichunguza unaweza kubaini kuwa pengine huwa unajiingiza katika kuwasema watu unapokuwa huna kazi,au unapokuwa na kundi fulani la watu.Tabia ya namna hii ni rahisi kujiepusha nayo,kwa kuepuka muktadha au mazingira husika.
Yawezekana unasumbuliwa na uvutaji wa sigara,ili uweze kuishinda tabia hii unapaswa kuepuka kukaa kwenye vijiwe vya wavutaji,pia na kutembea na kiberiti au na kiwashio kingine chochote.
Inawezekana isiwe rahisi kuiacha tabia,maana wakati mwingine unaweza kulazimika kuacha kitu cha maana mathalani,Wapo watu waliojizoesha kuvuta sigara wanapofanya kazi za kufikiria sana,kana kwamba wasipokuwa na sigara fikra hazitiririki.
Katika hali kama hii ambapo tabia iliyopendeza imekuwa sehemu ya jambo jingine muhimu,kinachotakiwa ni kuanza taratibu kuidhibiti tabia kabla ya kuiondoa.
- JENGA TABIA MBADALA ILIYO NJEMA
Hatua nyingine muhimu ya kuishinda tabia isiyofaa ni kujenga tabia mbadala,inayofaa.Kama una mazoea ya kunywa kahawa sana (na umeambiwa inakudhuru) anza kujenga utaratibu wa kutumia kitu kingine chenye manufaa zaidi,mathalani juisi aumatunda,kila unapohisi kuhitaji kahawa.
Hatua hii inaweza kuwa ngumu lakini ni vema mtu kuweka mizani na kupima hasara ya kuendelea kama alivyo na faida ya kubadilika.
Tabia inaweza kukomeshwa katika hali ya maisha uliyozoea kuishi,lakini tu kwa kuzingatia hatua hizi 4 .Nakukuhakikishia utajiweka katika hali nzuri ya kushinda tabia isiyofaa na hivyo kuuweka sawa mustakabaliwa maisha yako.
No comments:
Post a Comment