HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Friday, August 1, 2008

HELLEN KILLER ALIVYOUSHINDA MOYO WA KUKATA TAMAA




''...Kila wakati mlango mmoja wa furaha unapojifunga,mwingine hufunguka.Tatizo letu ni kwamba tunatumia muda mrefu kuutazama mlango uliojifunga ,kiasi kwamba hatuoni huo mlango mwingine wa furaha uliofunguka...''

Maneno hayo yalitamkwa na mhariri na mwanaharakati maarufu wa zamani wa haki za binadamu wa Marekani,Hellen Killer.Hellen Killer alikubwa na ugonjwa akiwa na umri wa miaka 19 tu na kujikuta akiwa kipofu na kiziwi.Hata hivyo ukiziwi na upofu haukumkatisha tamaa,kwani alisaka elimu hadi kuhitimu chuo kikuu cha RADCLIFE (MAREKANI) mwaka 1904.


Aliendelea kusoma hadi kufikia hatua za juu zaidi zilizomwezesha kuwa mhariri katika vyuo vikuu kadhaa vya Marekani.Alifariki mwaka 1968.Anakumbukwa duniani kama mmoja wa watu wa mwanzo kabisa wasiojiweza waliokataa kukwazwa na hali hiyo na waliochachamaa kutafuta maendeleo.

No comments: