Lazima mlo kamili uwe na viini lishe muhimu kwa binadamu,ikiwa kweli unataka ubakie na nguvu na hata muonekano wa ujana kwa muda mrefu.
Mlo kamili unatakiwa uwe na wastani wa asilimia 60 ya Wanga ( carbonhydrate ),asilimia 25 za Protini,na 25 za Mafuta.Kwa kawaida kiasi muhimu maana ni lazima kutumia aina fulani muhimu na sahihi za mafuta.
Ukweli ni kwamba upungufu wa aina hizo za mafuta husababisha matatizo mwilini,kama kisukari,shinikizo la damu,ugonjwa wa kusahau nk.
Omega -3 na omega -6 ni aina muhimu sana za mafuta.Aina hizi za mafuta hupatikana kwa wingi katika samaki mfano Salmon,kibua au kwenye karanga na soya.Lakini pia hupatikana kwenye mafuta ya mimea kama kwenye karanga,mafuta ya mahindi na Mzeituni.
Nafaka kama mahindi na mtama hutakiwa kuliwa bila kukobolewa,kwasababu virutubisho vyake huwa kwenye kile kinachoondolewa wakati kukobolewa.Unga unaotokana na nafaka zilizokobolewa hauna viini lishe bora kwa binadamu.
Unatakiwa kula Mboga mboga na matunda ya aina mbali mbali,ni vizuri kupata vibakuli kama 4 au 5 vya mboga mboga tofauti kwenye mlo wako wa kila siku.Mchanganyiko wa mboga mboga husaidia kujenga mwili kwa kuongeza virutubisho muhimu kwenye mwili wako,mboga za majani kama mchicha,kisamvu na venginevyo ni vizuri kutumia kwasababu zina vitamini nyingi kama zikitayarishwa vizuri.
Unapaswa pia ule jamii ya kunde,kama vile maharagwe,njegere nk.Pia samaki wana virutubisho muhimu kwenye mwili wa mwanadamu.
Asilimia 25 ya mboga za majani unazokula zinatakiwa kuliwa kama kachumbari,yaani bila kupikwa wala kuongezwa vitu vingi ndani yake,kwani huweza kupoteza umuhimu wake katika mwili.Lakini unaweza kuongeza vitu kama malimau ambayo yana Vitamin C inayohitajika mwilini.
Katika siku moja hakikisha umekula aina 2 au 3 za matunda,ikiwa mwili wako umezidi miaka 50 basi punguza ulaji wa mayai na bidhaa za nyama nyekundu.Pendelea zaidi kunywa maziwa haswa yasiyo na Lehema.
No comments:
Post a Comment