HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Thursday, February 19, 2009

JE UNAMFAHAMU MGUNDUZI WA BALBU

MZEE AKIWA KWENYE UTAFITI WAKE
ALIVYOKUWA DOGO,MTUNDU ASIYEPENDA KUTULIA SEHEMU MOJA

HII NI MASHINE YAKE YA KWANZA KUTENGENEZA INAITWA PHONOGRAPH



Thomas Alva Edson (11 Februari 1847 - 18 Octoba 1931) alikuwa mvumbuzi mashuhuri na mfanyabiashara nchini marekani. Aliboresha vifaa kama balbu ya umeme,mikrofoni na kugundua gramafoni. Utafiti na ufumbuzi wake ulihusu hasa mitambo ya umeme, lakini alijishughulisha pia na mtandao wa ugawaji wa umeme.

Edson alizaliwa katika familia ya Ohio kama mtoto wa 7, akasoma miezi michache tu shuleni na kufukuzwa kwasababu hakupenda kutulia sehemu moja na kusikiliza,akafundishwa na mama yake nyumbani. Aliugua mara kadhaa na alipokuwa na umri wa miaka 15, aliumwa karibu awe kiziwi.

Alipata kazi yake ya kwanza kwenye kampuni ya telegrafu, Kazi hii ilimwachia nafasi ya kujisomea na kutengeneza vifaa vyake vya kwanza. Alipokuwa na umri wa miaka 21 alitengeneza mashine ya kuhesabu na kukadiria kula kwenye chaguzi.

Mwaka 1877 aligundua mashine ya kushika sauti ikaitwa '' phonograph '' na kuwa mashine mama ya gramofoni.
Akaendelea kuboresha balbu ambayo hakuvumbua yeye lakini zilikuwa zinadumu kwa muda mdogo tu, Mwaka 1879 alifaulu kutengeneza balbu iliyotoa mwanga masaa 40 na baada ya miaka 3 alifanikiwa kuiboresha hadi kufikia masaa 1,000.

Edson alivumbua mengi na mapato yaliyotokana na mauzo ya mitambo yake, alijenga maabara kubwa, na kuajiri wahandisi na wasaidizi wengi.

Alitambua mapema ya kwamba kufaulu kwa mitambo ya umeme kulitaji mtandao wa usambazaji wa umeme. Aliendelea kutengeneza swichi na mita ya kuhesabu matumizi ya umeme.

Tangu 1881 kampuni ya Edison ilianza kuweka nyaya za umeme mjini New York na 1882 alimaliza kituo cha umeme cha kwanza. Hadi 1911 kampuni yake ilikuwa na vituo 33 vilivyotoa umeme kwa balbu milioni 4.6 na wateja 108,500. Kampuni yake iliendelea na kuwa kampuni kubwa iliyofahamika kwa jina la General Electric.

(Pamoja na mafanikio yote hayo katika kutengeneza balbu inasemekana alikosea zaidi ya mara 10,000 lakini hakukata tamaa)

No comments: