HAPA YUPO KENYA KUPATANISHA WAGOMBEA URAUS
Kofi Annan alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1996 - 2006. Alizaliwa 8 Aprili 1938 huko Kumasi,Ghana. Alipewa jina Kofi kuonyesha kuwa alizaliwa siku ya Ijumaa kuendana na utamaduni wa Ashanti. Jina Annan linamaanisha kuwa alikuwani mtoto wa nne kuzaliwa.
Mara baada ya kumaliza masomo ya Uchumi alijiunga na huduma ya Umoja Mataifa mwaka 1962 katika WHO. Mwaka 1974 - 1976 alifanya kazi Ghana halafu akarudi tena Umoja wa Mataifa. Akapanda ngazi kuwa makamu wa katibu mkuu mhusika wa usalama, aliwajibika kusimamia Shughuli za wanajeshi walio chini ya Umoja wa Mataifa.
Alihusika na Vita ya Rwanda pia ya Yugoslavia ambapo wanajeshi chini ya Umoja wa Mataifa alishirikiana.
Mwaka 1996 alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mwaka 2001 akarudishiwa tena cheo hicho hicho.
Mwaka 2008 Annan alirudi tena katika habari za kimataifa alipofika Kenya kwa shabaha ya kukutanisha viongozi wa kisiasa waliopingana juu ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa kenya mwaka 2007. Akasaidiana na Grace Machel na rais wa Tanzania Benjamini Mkapa. Aliendesha majadiliano kati ya wawakilishi wa ODM na PNU kwa muda wa wiki 5. Akafaulu kuleta mapatano ya ushirikiano kati ya pande zote mbili.
Kofi Annan ameoa mara ya pili. Mke wake Nane Maria Annan anatoka Uswidi na wana watoto watatu
No comments:
Post a Comment