HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Wednesday, February 18, 2009

JE UNAMFAHAMU JACOB ZUMA?



Alizaliwa katika familia ya kimaskini katika eneo la kwazulu-Natal. Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya apartheid (ubaguzi wa rangi wa kibaguzi). 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko Robben Island pamoja na Nelson Mandela.

Baada ya kuondoka gerezani akatoka Afrika kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC huko Msumbiji na Zambia. Aliingia katika uongozi hadi kuwa mkuu wa upelelezi wa ANC.

Tangu ANC kuhalalishwa tena katika Afrika Kusini mwaka 1990 Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama katika Natal na baada ya uchaguzi wa 1994 akawa waziri katika serikali ya kijimbo.

1997 alikuwa makamu wa mwenyekiti wa ANC na 1999 akateuliwa kuwa makamu wa rais wa jamhuri.

Mwaka 2005 mshauri wake Shabir Shaik alihukumiwa miaka 15 jela kwasababu alipokea rushwa,Zuma alishtakiwa pia na rais Thabo Mbeki akamwachisha katika serikali. Kesi hii ilisimamishwa kwasababu mashtaka hayakuandaliwa vizuri. Miezi michache baadaye alishtakiwa tena kwa kosa la madai ya kumnajisi mwanamke. Lakini kwa kesi hii Zuma hakuhukumiwa kwasababu hakimu alimwamini Zuma,maana mama yule aliwahi kukubali yote,yaani walikubaliana kufanya tendo hilo.
Mwaka 2007 Zuma akagombea nafasi ya mwenyekiti wa ANC dhidi ya Thabo Mbeki aliyetaka kuchaguliwa tena. Zuma alishinda, kwa sasa anagombea kiti cha urais,na Nelson Mandela anamsaidia katika kampeni.

No comments: