HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Tuesday, December 23, 2008

WAFAHAMU MARAISI WA UGANDA WALIVYOPATA UONGOZI KIMABAVU (SIR EDWARD MUTESA II, MILTON OBOTE, IDI AMINI DADA NA YOWERI MUSEVENI



IDI AMIN AKIBEBWA KIFALME NA WAFANYA BIASHARA WAINGEREZA HUKO KAMPALA

IDI AMINI AKIWA PAMOJA NA ASKOFU LUMUM, ALIYEUAWA BAADAYE KWA AMRI YAKE
Uganda ilipata Uhuru wake tarehe 9 Octoba 1962 kwa katiba ya Jamhuri yenye Serikali ya kibunge . Rais wa kwanza alikuwa Kabaka Sir Edward Mutesa II, na waziri mkuu Milton Obote.

Mwaka 1967 Obote alibadilisha katiba na kumfukuza Kabaka nchini.


Huyu ndiye Milton Obote, alizaliwa tarehe 28 Desemba 1925

MRS MILTON OBOTE



HAYA NDIO MAZISHI YA MILTON OBOTE







Mjue zaidi Obote kwa kubonyeza tovuti yake hapa chini:-

HISTORIA YA IDI AMINI DADA

Idi Amin Dada alikuwa rais wa Uganda kati ya mwaka 1971 hadi mwaka 1979 aliyetawala kama dikteta. Historia yake jinsi alivyojipenyeza na kufanikiwa kupindua nchi, kwanza alikuwa mwanajeshi wa kawaida akapanda ngazi na kuwa jenerali na mkuu wa jeshi la Uganda. Mwaka 1971 alimpindua rais Milton Obote akajitangaza kuwa rais mpya.

Mara moja alianza kuwatesa wafanyakazi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makidirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka 4 ya utawala wake.

Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa ni kufukuzwa kwa watu wote wenye asili ya kihindi, na kugawa maduka na biashara zao kwa ndugu na wafuasi wa rais. Takribani watu 80,000 walipaswa kuondoka, wengi wao walihamia Uingereza, Marekani na Kanada hasa.

Octoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius .K. Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tarehe 11 Aprili 1979.

Amini alitoroka Libya, halafu Iraq na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutokujishughulisha na siasa tena. Alikufa mjini Jeddah Tarehe 16 Agosti 2003.

Alizaliwa tarehe 19 Novemba 1924 na kufariki 21 Novemba 1969


Yoweri Museven


Tembelea tovuti yake
www.sudantribune.com/spip.php?article26951

Mara baada ya Amini kuondoka, Uchaguzi wa mwaka 1980 Ulimrudisha Obote Serikalini, aliyeanzisha upya uditecta na kuua watu hovyo. Wapinzani wake wakiongozwa na Museven,walirudi polini wakashika silaha katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kundi la Museven likashinda na kutwaa serikali tangu mwaka 1986.

Museven alichaguliwa kuwa Rais katika kura bila vyama vya upinzani mwaka 1996 na 2001. Mwaka 2005 kulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi kwa mara ya kwanza. Museven alipata kibali cha Bunge kwa badiliko la katiba lililomruhusu kugombea urais tena mwaka 2006 akachaguliwa kwa mara ya 3

No comments: