The British Broadcasting Corporation (BBC) ni shirika la utangazaji la Uingereza. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1922 kwa jina la British Broadcasting Company Ltd kama kampuni binafsi. Baadaye mwaka 1927 lilibadilishwa hadhi yake na kuwa shirika la umma. BBC ndio shirika la habari kubwa kuliko yote duniani likiwa linatoa habari na taarifa mbali mbali kwa njia ya redio, Luninga na Internet.
Kwa mujibu wa BBC, lengo lake ni kutoa habari, kuelimisha na kuburudisha. Kauli mbiu yake ni '' Nation Shall Speak Peace Unto Nation '' .
Shirika hili linaongozwa na bodi ya Magavana wanaochaguliwa na Malkia au Mfalme wa Uingereza kwa ushauri toka kwa Waziri wa Serikali ya Uingereza. Hata hivyo, BBC inasema katika katiba yake, kuwa inafanya kazi zake bila shinikizo toka kwa wanasiasa au wafanyabiashara na kuwa na kuwa linawajibika kwa wasikilizaji na watazamaji wake tu.
Tembelea tovuti yao ;-
No comments:
Post a Comment