Shaka alikuwa mtoto wa Chifu Senzangakhona ka Jama na Nandi binti wa chifu wa Langeni. Jina lake ni kutokana na neno la Kizulu '' Ishaka '' linalomtaja mdudu ambaye katika imani ya utamaduni wa Kizulu anasemekana kuvuruga hedhi ya wakina mama. Jina hili ni dalili ya kuzaliwa nje ya utaratibu. Hivyo miaka ya kwanza ya Shaka ilikuwa miaka migumu bila baba anayejulikana rasmi na akijisikia kudharauliwa na watu wengine. Utoto huu ulisababisha hasira ndani yake na baadaye alilipiza kisasi.
Kama kijana Shaka alikuwa wa kabila kubwa zaidi la Mthethwa alipoingia pamoja na hirima yake katika jeshi. Wakati ule Ukoo wa Wazulu walikubali wamthehtwa kuwa mabwana wao. Chifu wa Mthethwa alikuwa Dingiswayo, aliyeanzisha utaratibu mpya wa Impi yaani kupanga watu wake vitani katika vikundi na kuwa na ngazi mbali mbali za mamlaka. Shaka alihudumia miaka 6 katika vita za Dingiswayo akawa hodari sana na kujifunza uongozi alioboresha baadaye.
Baada ya kifo cha baba yake, Shaka Zulu alirudi kwa Wazulu kwa msaada wa Dingiswayo akachukua uongozi mnamo mwaka 1812. Baada ya kuwa kiongozi akalipiza kisasi kwa maadui wa utotoni akiwaua kwa njia mbali mbali.
Shaka aliendelea kukubali Ubwana wa Mthethwa na Dingiswayo hadi huyu aliuawa vitani na kabila la Ndwandwe mwaka 1817. Lakini pamoja na hayo alipigana vita na ukoo na makabila madogo ya jirani. Mbinu yake ilikuwa ni kuwashambulia waliompinga na kuwa hatari kwao, wanawake na watoto waliingizwa katika ukoo wake, pamoja na wanajeshi wa kiadui walionusurika kuuawa lakini ni kwa wale waliokubali kumfuata baada ya kushindwa. Kwa njia hiyo ukoo mdogo wa kizulu uliendelea kukua.
Baada ya kifo cha Dingiswayo mwaka 1817, Shaka alishambulia kabila kubwa la Ndwandwe akawashinda kwenye mapigano ya kilima cha Gqokli kwa sababu ya mbinu zake za kijeshi ingawa idadi ya watu wake ilikuwa nusu tu ya adui.
Katika miaka iliyofuata Shaka aliendelea kushambulia vikundi vya jirani na kuwaingiza kwenye utawala wake. Makabila mengine walimfuata bila vita na kukubali uongozi wake,na kuingiza vijana wao katika Impi au vikosi vya Shaka. Alituma viongozi au majenerali wake pamoja na Impi pande mbali mbali mpaka Msumbiji na Zimbambwe. Vikundi kama ndebele huko Zimbambwe au hata Wangoni katika Tanzania ni matokeo ya matembezi ya Impi za Kizulu zilizoenda mbali na kupoteza mawasiliano na nyumbani.
Vita hivi vilisababisha makabila mengine kukimbia na kuhama hama na kushambulia majirani zao hivyo kupanusha eneo la vita katika nchi mbali na Wazulu wenyewe. Kipindi hiki kinakumbukwa kwa majina kama '' Mfekano ' (Kizulu) au '' Difaqane (Kisotho) kuwa miaka 30 ya vita na vifo.
Katika mawazo ya wataalamu, Shaka aliandaa upanuzi wa Makaburu kwa uharibifu wa vita zake. Makaburu walipoanza kuenea ndani ya Afrika Kusini walikuta maeneo mazuri bila watu, lakini magofu kuonyesha kuwa watu wameshawahi kuishi hapa. Pamoja na hayo makabila mengine kama Wasotho, Waswazi, Wandebele au Wagaza walioshambuliwa walijifunza mbinu za kijeshi na kufaulu kujitetea na kuanzisha mataifa makubwa yakiunganisha wenyewe koo na makabila madago zaidi.
Utawala wa Shaka ulikuwa wa tabia za kinyama zilizosababisha chuki nyingi dhidi yake. Baada ya kifo cha mama yake nandi alikuwa na hasira kiasi cha kuua watu 7000 kati ya wanajeshi wake kwa kosa la kutoonyesha huzuni ya kutosha na kuamuru kipindi cha kufunga miezi 3. Aliamuru mashamba yasilimwe kwa mwaka 1 , na kila mwanamke asionekane kuwa na mimba, katika kipindi hiki aliwaua wote waliokuwa wajawazito pamoja na mumewe. Wataalamu wengine huona wakati ule shaka alikuwa na kichaa.Maadui walifanya mpango dhidi yake mwishowe aliuawa na ndugu zake. Mwaka 1828 Impi nyingi zilikuwa mbali vitani ikuli ikawa bila ulinzi wa kutosha. Kaka zake Dingane na Mhlangalangana walimuua nakutupa maiti yake shimoni
1 comment:
Ahsante kwa ku kopy na ku paxte kene wkpedia
Post a Comment