Radio ni chombo (kifaa) kinachopokea mawasiliano kutoka katika kituo cha redio na kuyabadilisha kuwa sauti. Kwa kawaida redio inapokea kwa njia ya antena yake mawimbi sumaku umeme yanayosambazwa na antena ya kituo cha redio. Kuna pia aina za redio ambako mawasiliano hufika kwa umbo la alama za umeme katika waya. Mawasiliano ya sumaku umeme yanasambazwa pia kwa njia ya chombo anga au satelaiti lakini njia hii inahitaji vyombo maalum na antena ya kawaida haitoshi
Huyu ni Heinrich Hertz aliyegundua mawimbi ya radio, alizaliwa tarehe 22 Februari 1857 katika mji wa Hamburg - Ujerumani na kufariki 1 Januari 1894 katika mji wa Bonn - Ujerumani akiwa na umri wa miaka 37.
Huyu naye alishiriki kuendeleza pale Heinrich alipofikia, anaitwa Guglielmo Marconi alizaliwa tarehe 25 Aprili 1874 huko Italia na kufariki tarehe 20 Julai 1937. Pia alishawahi kuwa mshindi wa tuzo ya Nobel.
Huyu naye pia alishiriki, anaitwa Nikola Tesla alizaliwa tarehe 10 Julai 1856 katika mji wa Hungary - Australia na kufariki tarehe 7 Januari 1943 huko New York - Marekani, akiwa na umri wa miaka 86.
IFAHAMU SASA HISTORIA FUPI YA RADIO
HISTORIA YA RADIO
WAJUE WATU WALIOSHIRIKI KUVUMBUA TEKNOLOJIA YA RADIO
Huyu ni Heinrich Hertz aliyegundua mawimbi ya radio, alizaliwa tarehe 22 Februari 1857 katika mji wa Hamburg - Ujerumani na kufariki 1 Januari 1894 katika mji wa Bonn - Ujerumani akiwa na umri wa miaka 37.
Huyu naye alishiriki kuendeleza pale Heinrich alipofikia, anaitwa Guglielmo Marconi alizaliwa tarehe 25 Aprili 1874 huko Italia na kufariki tarehe 20 Julai 1937. Pia alishawahi kuwa mshindi wa tuzo ya Nobel.
Huyu naye pia alishiriki, anaitwa Nikola Tesla alizaliwa tarehe 10 Julai 1856 katika mji wa Hungary - Australia na kufariki tarehe 7 Januari 1943 huko New York - Marekani, akiwa na umri wa miaka 86.
IFAHAMU SASA HISTORIA FUPI YA RADIO
Mwaka 1886 Mjerumani Heinrich Hertz alitambua mawimbi ya sumakuumeme. Wataalamu na wahandisi mbali mbali walifanya majaribio katika miaka inayofuata kutumia mawimbi haya kwa mawasiliano, Kati yao ni Mwitaliano Guglielmo Marconi, Mwamerika Nikola Tesla na Mrusi Alexander Popov. Kila mmoja ametajwa kama '' mtu wa kwanza aliyegundua radio ''.
Kituo cha kwanza cha radio kianzishwa na Mholanzi Hanso Schotanus a Steringa Idzerda tarehe 06 Novemba 1919 aliposambaza mawimbi ya muziki kutoka nyumbani kwake. Kituo cha kwanza cha biashara kilianza kazi mwaka 1920 Marekani mjini Pittsburgh.
Katika miaka iliyofuata redio ilisambaa duniani kote duniani. Ni njia muhimu ya kusambaza habari pamoja na utamaduni hasa muziki
No comments:
Post a Comment