MCHAWI AZIKWA AKIWA HAI PAMOJA NA MAREHEMU ALIYEDAIWA KUMUUWA KWA USHIRIKINA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni
Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai
wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo. Tukio
hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu majira ya Saa Nane
Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga
aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya
Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema marehemu
alipatwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye
jina lake halikuweza kujulikana maramoja. Amesema wakati taratibu za
mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu
kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za
kishirikina. Ameongeza kuwa wakati
kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika marehemu ndipo vijana waliokuwa
wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike makaburini kwa ajili ya
kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa Kaburi ambalo
lilikuwa limekwisha chimbwa. Kutokana na mwito huo walifika wazee
wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na
kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia
kaburini huku akisindikizwa na marungu.. (Habari zaidi na
No comments:
Post a Comment