MH Lowasa akiwa na Familia yake Mkewe Regina Lowasa na Binti Yao
Katika kutekeleza mkakati huo, Januari mwaka huu, Lowassa alijitokeza kuzungumzia vurugu zilizotokea mkoani Arusha zilizotokana na mvutano katika uchaguzi wa meya wa jiji hilo kati ya CCM na CHADEMA.Katika mnyukano huo, watu watatu walipigwa risasi na polisi na kufariki dunia baada ya polisi kutumia nguvu isiyo ya kawaida kuzima maandamano ya CHADEMA.Kauli hiyo ya Lowassa ilikuwa tofauti na msimamo wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtaka kuwasilisha maoni yake katika vikao vya chama badala ya kutumia vyombo vya habari.Kauli nyingine ya Lowassa ilihusu nyongeza ya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi, kutokana na kile alichoita mfumuko wa bei kuwa mkubwa.Bali wiki moja iliyopita, Naibu Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mganya alimtuhumu Lowassa kwa kutoa kauli hiyo akisema ana ajenda ya siri nyuma yake.Mgaya alisema TUCTA haihitaji msaada wa Lowassa katika kusimamia madai yao. Alisema “mbunge huyo wa Monduli inaonekana ana ajenda yake mgongoni.”Hatua nyingine ya Lowassa katika kujikarabati kisiasa ni kugombea na kupata nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.Lowassa amekuwa pia akihudhuria hafla nyingi, hasa za madhehebu ya Kikiristo (KKKT) ambao anaonekana akitoa maoni mbalimbali kama ilivyokuwa Jumapili iliyopita ukumbi wa Dimaond Jubilee kwenye uzinduzi wea albamu ya moja ya kwaya za injili.Kwenye kusanyiko hilo, Beatrice naye alikuwepo. Lowassa alimtaka asome maoni ya gazeti la The Citizen juu ya ushirikina uliokithiri nchini; jambo ambalo Lowassa alizungumzia kwa urefu.MwanaHALISI lilipowasiliana na Beatrice ili kupata maoni yake juu ya ushwahiba wake mpya na Lowassa, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:Mwandishi: Tusaidie maelezo kidogo juu ya ujumbe uliomwandikia Mheshimiwa Pindi Chana kumjulisha kuwa uliambiwa Edward Lowassa atakuwa rais. Ni kweli?Beatrice: Barua ameandika nani na umeipata wapi?Mwandishi: Hii barua fupi – memo ndani ya Bunge, uliposema Mheshimiwa Lowassa ambaye amesimamia vizuri kura zako za ukamishna wa Bunge.Beatrice: Sina taarifa hiyo. Wala siikumbuki. Unajua ndani ya Bunge tunaandikiana mambo mengi, tena mengine ya utani tu. Na mimi na Mheshimiwa Chana sote ni “walokole,” tunafanyiana utani sana.Mwandishi: Kwani mheshimiwa Shelukindo, mkiwa ndani ya bunge kuna utani mwingi, kwamba huwa mnaandikiana utani sana?Beatrice: Kabisa, unajua tunaandika mambo mengi. Na kama unaandika kwa utani kwa mwenzako inabaki hivyo ni utani tu. Sasa tatizo hao wanaowaletea mambo haya wanatumia mambo haya kutafuta mipango yao ya kufikia mwaka 2015.Alisema, “Mimi najua hakuna anayenibeba ndugu yangu. Mimi ni very solid (ngangari), sibebeki. Nakwambia, mbona mimi nina nguvu nyingi mimi mwenyewe; sihitaji kubebwa. Najua wanajaribu kuonyesha tunabebwa, lakini huo ni ujinga wao wa kufikiri.Mwandishi: Mheshimiwa Shelukindo, kwani nyie waheshimiwa huwa mnatafutana (kufitiniana)?Beatrice: Hiyo inafanyika sana, watu wakishakuwa na mambo yao wanatumia wengine kutimiza dhamira zao. Lakini mimi ninafikiria wananchi. Nimeshaamua kwamba Beatrice nashughulikia shida za wananchi jimboni. Ninatafuta njia za kuwaondolea umasikini, njaa na mambo kama hayo. Sasa wengine wanatafuta tu pa kunishika.Mwandishi: Kwa hiyo Mh. Lowassa ndiye alikuwa kampeni meneja wako katika kutafuta ukamishna pale bungeni, au siyo Mheshimiwa?Beatrice: Lakini kama anafanya kazi ya kampeni vizuri; ni vizuri tu. Isipokuwa kila mtu anajichukulia mwenyewe alivyo. Mimi ni mtu wa kazi sihitaji kusimamiwa hivyo. Na hebu tujadili hili; unajua kaka nyinyi mnafanya kazi kubwa. Sasa hii kusikia, sijui MwanaHALISI hivi, sijui hivi, pengine kuna watu wanachomekea vitu vyao. Tunapenda kazi yenu.Mwandishi: Mheshimiwa nakushukuru sana.Beatrice: Karibu sana tutafanya kazi pamoja.Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, mume wa Beatrice, William Shellukindo, alikuwa na msimamo mkali dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini na hiyo ndiyo inayoelezwa kuwa sababu ya kushindwa kwake ubunge katika mchakato wa ndani ya CCM.
Shellukindo alikuwa mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga kwa zaidi ya miaka 20, alishindwa katika kura za maoni na January Makamba, mtoto wa katibu mkuu wa CCM anayetajwa kuwa mfuasi wa mtandao wa Lowassa.
No comments:
Post a Comment