Wanaume wawili, Athumani Hamis ‘Anti Asu’ na mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Ally wakazi wa jijini Dar es Salaam waliodaiwa kufunga ndoa hivi karibuni katika eneo la Sinza, wamelaaniwa vikali kutokana na uamuzi huo ambao unakwenda kinyume na maadili ya nchi.Wakiongea na Risasi Jumamosi mara baada ya ndoa hiyo kuripotiwa kwenye vyombo vya habari, baadhi ya watu walisema kuwa, wameshangazwa na tukio hilo ambalo hawakutarajia kama lingeweza kutokea Tanzania na kuungwa mkono.Walisema kuwa, vitendo vya kishoga havikubaliki katika jamii yoyote hivyo imefika wakati serikali kuingilia kati na kuhakikisha wanaofanya hivyo wanachukuliwa hatua kali."Hawa wanaume waliooana Mungu awalaani, huu ni uchafu usiovulimika, iweje mwanaume amuoe mwanaume mwenzake wakati wanawake wanaotafuta waume wamejazana? Wakati umefika wa serikali kuwashughulikia na kama watashingwa sisi tutadili nao,"alisema Hamza Salehe wa Tandale kwa Mtogole.Alisema kuwa, Anti Asu na Ally ni mfano tu wa wanaume wengi ambao hivi sasa wanaishi kama mke na mume kwani katika eneo analoishi wapo mashoga wengi na wengine wana wapenzi bila kificho.Naye Mama Kassim wa Buguruni Malapa alizilaani ndoa za jinsia moja, si kwa wanaume tu bali hata wanawake ambao nao wamekuwa wakiwekana kinyumba kinyemela."Ni vitendo visivyowavutia wengi, achilia mbali hawa wanaume, kuna wanawake wanaofanyiana vitendo vya kisagaji na mwisho wa siku kuishi kama mke na mume, sisi tunawalaani wanaofanya hivyo lakini serikali ilivalie njuga suala hili,"alisema Mama Kasim.Vitendo vya kishoga vimekuwa vikishamiri Bongo hali inayowafanya baadhi ya watu kuhofia kwamba, tuendako inawezekana ikaonenaka ni kawaida watu wa jinsi moja kuoana, kitu ambacho ni hatari.
No comments:
Post a Comment