HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Monday, December 15, 2008

MFAHAMU RAIS GEORGE W. BUSH


George W.Bush ni mtoto wa rais mstaafu wa marekani aitwaye George H. Bush aliyetala Marekani kati ya mwaka 1989 - 1993, alizaliwa tarehe 6 Julai,1946 katika jimbo la Connecticut huko Marekani,elimu yake ya Chuo kikuu aliipata katika Chuo kiitwacho Yale. Hakushiriki katika vita ya Vietnam lakini alijiandikisha kati ya wanamgambo wa jimbo la Texas.

George W. Bush ni mwenyeji wa jimbo la Texas alipokuwa Gavana kabla ya kugombea urais, Mwaka 2000 aligombea Urais kwa kupitia chama cha Republican. Alishinda kufuatana na azimio la mahakama kuu kwa sababu kura ya jimbo la Florida haikueleweka vizuri na kwa jumla kura zake zilikuwa karibu sawa na zile za mpinzani wake Al Gore.

Vipindi 2 vya Bush viliathiriwa sana na mashambulio ya tarehe 11 Septemba 2001. Baada ya shambulio hilo la AL Qaida Bush aliamuru vita dhidi ya Alghanistan ambako magaidi walikuwa wamekimbilia huko na kujificha.

Mwaka uliofuata Bush aliamua kwa sababu sizizoeleweka vema kushambulia pia Iraq ingawa Iraq haikushiriki katika mashambulio ya Septemba 11 wala kuwa na uhusiano na Al Qaida.

Mwanzoni Marekani pamoja na msaada wa Uingereza ilifaulu vema kulishinda jeshi la Iraq na kumpindua diktecta Saddam Hussein. lakiniushindi huu uligeuka kuwa vita ndefu ya wanamgambo wa Iraq dhidi ya Marekani. Watu wengi waliiendelea kufa na vita hii iliharibu sifa za Bush

No comments: