HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Tuesday, December 16, 2008

MFAHAMU LEO MUAMMAR AL-GADDAFI NA MFALME IDRIS I ALIYEMPINDUA


MUAMMAR AL-GADDAFI

Amiri Muammar al-Gaddafi ni kiongozi wa taifa la Libya. Amezaliwa katika familia ya Mabedawi (wafugaji wahamiaji) mnamo mwaka 1942. Mara baada ya kumaliza masomo yake ya sheria kwenye chuo kikuu cha Libya,alijiunga na jeshi mwaka 1963 akasoma kwenye chuo cha kijeshi cha Sandhurst (Uingereza) mwaka 1965.

Tarehe 1 Septemba 1969 pamoja na maafisa wenzake alipindua Serikali ya Mfalme Idris I na kutangaza Jamhuri ya Kiarabu ya Libya. Ingawa hana cheo rasmi lakini anaendelea kutawala nchi yake akiitwa '' kiongozi wa mapinduzi ya 1 septemba ya Jamuhuri ya ujamaa ya watu wa Kilibya - Kiarabu ''.



MARA BAADA YA KUMFAHAMU KWA UFUPI MUAMMAR AL-GADDAFI SASA MFAHAMU MFALME MOHAMMAD IDRIS I, ALIYEPINDULIWA NA AL-GADDAFI.
MUHAMAD IDRIS I
Idris I (12 Machi 1890 - 25 Mei 1983) alikuwa mfalme wa kwanza wa Libya kati ya mwaka 1951 mpaka 1969.
Jina lake la kiraia alikuwa akiitwa Muhamad Idris bin as-Sayyid ibn Muhamad as-Senussi. Alikuwa mjukuu wa Muhamad ibn Ali as-Senussi aliyeanzisha jumuiya ya Wasufi wa Senussi. Muhamad alirithi cheo cha babu yake. Akakubaliwa kama emir wa Cyrenaike na Uingereza na Italia baada ya vita kuu ya kwanza ya Dunia. Baada ya Italia kuvamia Libya aliongoza vita ya porini.

Tangu mwaka 1951 aliongoza Taifa jipya la Libya. Mwaka 1969 alipinduliwa na wanajeshi chini ya uongozi wa Muammar al-Gaddafi. Alikufa Misri uhamishoni mwaka 1983

No comments: