ALBINO WA KIHINDI
ALBINO WA KIZUNGU AMBAYE NI DOKTA
SASA MARA BAADA YA KUGUNDUA HAWA NI NDUGU ZETU NI WATU KAMA MIMI NA
WEWE, KWANINI TUNAWAFANYA NI CHANZO CHA KUPATA UTAJIRI,KUFANIKIWA HAKUJI KWA KUMWAGA DAMU YA MWENZAKO
Huyu mama alikatwa mkono,watu wakakimbia nao,inasemekana nyumba yao ilizingirwa na kundi la watu wenye nia moja ya kudhuru ili wafanikiwe,wakafanikiwa kuvunja mlango wakamkamata na kumkata mkono wake wa kulia.Alipopiga kelele ndugu zake wakaja akawaambia aliyenikana nimemuona,namfahamu na ni jirani yetu.Walipomkimbilia wakamkuta huyo mtuhumiwa akiwa anatetemeka na amelowa damu.
KAMA HIYO HAITOSHI FUATILIA HAWA WATOTO WALIVYO KATWA MIKONO NA KUCHARAZWA MAPANGA
KAMA HIYO HAITOSHI FUATILIA HAWA WATOTO WALIVYO KATWA MIKONO NA KUCHARAZWA MAPANGA
Jeshi la polisi Mkoani Kagera,linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Kagoma Wilayani Biharamuro,huku wakiwasaka wengine 2,kwa tuhuma za kumkata mtu mmoja ambaye ni Zeru zeru na kutoweka nao huku wakimuacha akiwa hai.
Kamanda Msika alisema wakati mtoto huyo akiwa nje ya nyumba akiota moto,huku mama yake mzazi akiwa ndani akipika chakula chakula,ghafla walitokea watu 3 wakiwa na mapanga na kuanza kumshambulia mtoto huyo kichwani ambako kama vile haitoshi,mmoja wao aliushika mkono wake wa kushoto na kuukata na kisha kukimbia na mkono huo
Imeelezwa kuwa kelele zilizopigwa na mtoto huyo zilimshtuma mama yake mzazi hali iliyomfanya atoke ndani ya nyumba,na wakati anafika nje alifanikiwa kumuona mmoja mmoja wa watuhumiwa hao, ambaye alimtambua kwa jina la Zakaria Petro ( 30) wakati akirudi kuuchukua mkono wa mtoto huyo uliodondoka wakati za purukushani za kukimbia
Habari zinaeleza kwamba mama huyo alimchukua mtoto wake ambaye alikuwa akivuja damu nyingi na kumkimbiza hospital na kisha kwenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi.
Baada ya taarifa kufika Polisi ulitembezwa msako mkali na Mtuhumiwa Zakaria kukamatwa na sasa wanawasaka watuhumiwa waliobaki.
Hili ni tukio la 3 kutokea katika mikoa ya kanda ya ziwa katika kipindi kisichozidi wiki 3,ambapo katika tukio la kwanza huko mkoani mara,zeru zeru mmoja aliuwa kwa kuchinjwa na kisha watuhumiwa wakatoweka na baadhi ya viungo vyake.
Siku chache baadaye tukio kama hilo likatokea katika wilaya ya kwimba Mkoani Mwanza ambako mtoto mwingine ambaye ni zeru zeru alikamatwa na watu wasiofahamika na kumchinja,kisha kutoweka na baadhi ya viungo vyake huku wakitelekeza mwili wake
JE NI NANI ANASABABISHA HILI?
Vyombo vya habari na Polisi winasema waganga wa kienyeji,wengine ukata wa maisha.Lakini mimi nadhani ujinga na ufisadi ndio unaochangia.Maana mafisadi wanasababisha maisha kuwa magumu.
ACHA KUUA ALBINO NI BINADAMU KAMA WEWE HANA KITU CHA KUSABABISHA UWE TAJIRI
No comments:
Post a Comment