Lazima Mlo kamili uwe na viini Lishe muhimu kwa binadamu,ikiwa kweli unataka ubakie na nguvu na hata mwonekano wa ujana kwa muda mrefu.
Mlo mkuu unatakiwa unatakiwa uwe na wastani wa asilimia 60 ya Wanga (carbonhydrate),asilimia 25 ya protini na 25 ya mafuta.Kwa kawaida kiasi muhimu cha mafuta kinachohitajika mwilini hakiwezi kuzalishwa na mwili wenyewe,ndio maana ni lazima kutumia aina fulani muhimu na sahihi za mafuta.
Ukweli ni kwamba upungufu wa aina hizo za Mafuta husababisha matatizo mwilini,kama Kisukari,Shinikizo la damu,Ugonjwa wa kusahau n.k.
Omega -3 na Omega -6 ni aina muhimu sana za mafuta.Aina hizi za mafuta hupatikana kwa wingi katika Samaki mfano Salmon,Kibua au kwenye karanga ya Soya.Lakini pia hupatikana kwenye mafuta ya mimea kama kwenye Karanga,Mafuta ya Mahindi na Mzeituni.
Nafaka kama mchele na mtama hutakiwa kuliwa bila kukobolewa,kwasababu virutubisho vyenyewe huwa kwenye kile kinacho ondolewa wakati wa kukobolewa.Unga unaotokana na nafaka zilizokobolewa hauna viini lishe bora kwa binadamu.
Unatakiwa kula Mboga na matunda ya aina mbalimbali.Ni vizuri kupata kupata vibakuli kama 4 au 5 vya mboga mboga tofauti kwenye mlo wako wa kila siku.Mchanganyiko wa mboga husaidia kujenga mwili kwa kuongeza virutubisho muhimu ndani ya mwili wako.Mboga za majani kama mchicha,kisamvu na nyenginezo ni nzuri kutumia kwasababu zina vitamini nyingi kama zitatayarishwa vizuri.
Unapaswa pia ule vitu aina ya kunde,kama vile maharagwe,njegere na kadhalika.samaki pia wana virutubisho muhimu kwenye mwili wa binadamu.
Asilimia 15 ya mboga za majani unazokula zinatakiwa kuliwa kama kachumbari,yaani bila kupikwa wala kuongeza vitu vingi ndani yake,kwani huweza kupoteza umuhimu wake katika mwili.lakini unaweza kuongeza vitu kama malimaun ambayo yana vitamini C inayohitajika mwilini.
Katika siku moja hakikisha umekula aina mbili au tatu za matunda,ikiwa umri wako umezidi miaka 50 basi punguza ulaji wa mayai na bidhaa za nyama nyekundu.Pendelea zaidi kunywa maziwa haswa yasiyo na Lehema.
WAJUE MAWAZIRI WAKUU TANGU UHURU DESEMBA 9,1961
NO.1 MW:JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Huyu ni Mwalimu Julius Kambarage nyerere ,alizaliwa Aprili 13,alikuwa mtoto wa Chifu Nyerere Burito wa Wazanaki,alianza shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 12.Baada ya kupata elimu ya msingi Musoma,alikwenda Tabora kwa masomo ya sekondaBaadaye alikwenda Makerere,Uganda ambako alipata stashahada ya elimu.Aliporejea alifundisha shule ya St.Mary's Tabora kwa sasa Milambo sekondari.Mwaka 1949 alikwenda Edinburgh ambako alihitimu Stashahada ya Uzamili katika Uchumi na Historia.Aliporejea aliacha kazi ya ualimu na kuongoza harakati za kugombania Uhuru chini ya chama cha TAA na baabaye TANU.Alifanikiwa kuun'goa utawala wa Waingereza na kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru mwaka Desemba 9,1961.Alifariki dunia Octoba 14,1999 katika hospital ya Mtakatifu Thomas,Uingereza kwa tatizo la saratani ya damu.
NO.2 RASHID MFAUME KAWAWA.
Songea Mkoani Ruvuma.Alisoma elimu ya msingi Liwale Lindi Mwaka 1941 hadi 1942 na baadaye kujiunga na elimu ya
NO .3 EDWARD MORINE SOKOINE
sekondari Dar es salaam.Mwaka 1962 aliteuliwa kuwa waziri mkuuhadi mwaka 1977.
Alizaliwa mwaka 1938 Monduli mkoani Arusha,alikuwa waziri mkuu wa 3 tangu Tanzania ipate Uhuru,aliapishwa kushika madaraka hayo Februari 13 mwaka 197Alitumikia nafasi hiyo hadi Novemba 7,1980 alipojiudhuru kwa muda na kwenda masomoni.
sekondari Dar es salaam.Mwaka 1962 aliteuliwa kuwa waziri mkuuhadi mwaka 1977.
Alizaliwa mwaka 1938 Monduli mkoani Arusha,alikuwa waziri mkuu wa 3 tangu Tanzania ipate Uhuru,aliapishwa kushika madaraka hayo Februari 13 mwaka 197Alitumikia nafasi hiyo hadi Novemba 7,1980 alipojiudhuru kwa muda na kwenda masomoni.
Alirejea tena kwenye wadhfa huo Februari 24 mwaka 1983.Alitumika nafasi hiyo hadi aprili 12,1984 alipofariki katika ajali ya gari akiwa safarini kutoka Dodoma kuelekea Dar es salaam baada ya kuhairishwa kwa mkutano wa Bunge.
NO.4 CLEOPA DAVID MSUYA
Alizaliwa mkoani kilimanjaro Novemba 4,1931.Aliapishwa kushika nafasi hiyo Novemba 19880 hadi February 24,1983.Akatumikia tena wadhifa huu kuanzia Desemba 7,1994 hadi Novemba 28,1995
NO. 5 DKT:SALIM AHMED SALIM
Alizaliwa January 23,1942 kisiwani Pemba.Aliapishwa kushika wadhifa huo April 24 mwaka 1984 kufuatiwa kifo cha waziri mkuu,Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Alitumikia nafasi hiyo hadi novemba 5,1985.Mbali na wadhifa huo Dkt Salim amekuwa mwana Diplomasia wa kutukuka kuanzia miaka ya 1960.Miongoni mwa ngazi za juu alizofikia katika nyanja hiyo,ni pamoja na kuwa balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.Rais wa baraza kuu la umoja wa mataifa,aliwahi kugombea nafasi ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa na alikosa kutokana na mizengwe ya nchi za magharibi.
Alizaliwa January 23,1942 kisiwani Pemba.Aliapishwa kushika wadhifa huo April 24 mwaka 1984 kufuatiwa kifo cha waziri mkuu,Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Alitumikia nafasi hiyo hadi novemba 5,1985.Mbali na wadhifa huo Dkt Salim amekuwa mwana Diplomasia wa kutukuka kuanzia miaka ya 1960.Miongoni mwa ngazi za juu alizofikia katika nyanja hiyo,ni pamoja na kuwa balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.Rais wa baraza kuu la umoja wa mataifa,aliwahi kugombea nafasi ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa na alikosa kutokana na mizengwe ya nchi za magharibi.
Dkt Salim pia alikuwa katibu mkuu wa uliokuwa wa uliokuwa Umoja wa nchi huru za kiafrika(OAU) kwa vipindi 3 mfululizo.
NO. 6:JOSEPH SINDE WARIOBA
Jaji Joseph Warioba alizaliwa Septemba 3,1990,Nyamswa,Bunda mkoani Mara.Aliingia madarakani Novemba 5,1985 katika utawala wa awamu ya pili wakati wa utawali wa Rais Ali Hassani Mwinyi.
Alitumikia wadhifa huo hadi Novemba 9,1990.Jaji Warioba amewahi kushika nyadhifa mbali mbali Kitaifa na Kimataifa katika fani yake ya sheria ikiwa ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia mipaka ya Bahari.
Alizaliwa mwaka 1934,Bugiri Mkoani Dodoma.Alishika madaraka hayo Novemba 9,1990 hadi Desemba 7,1994.Baada ya kuondoka nafasi hiyo ilichukuliwa tena na Bw.Cleopa Msuya hadi mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.Kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 1997 alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara.
NO.8:FREDERICK TLUWAY SUMAYE
Alizawa mwaka 1950,Mkoani Manyara.Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza tangu ulipofanyika Uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania.Alishika nafasi hiyo Novemba 28,1995 hadi Desemba 3,2005.
Alizawa mwaka 1950,Mkoani Manyara.Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza tangu ulipofanyika Uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania.Alishika nafasi hiyo Novemba 28,1995 hadi Desemba 3,2005.
NO.9: EDWARD NGOYAI LOWASA
Alizaliwa Mwaka 1953 Monduli Mkoani Arusha.Aliapishwa kushika wadhifa huo Desemba 30,2005,ametumikia wadhifa huo hadi Februari 7,2008.
Aliachia madaraka hayo kwa kujiuzulu mwenyewe,ambapo alisema katika Ukumbi wa Bunge anafanya hivyo ili kulinda heshima yake, kutokana na kashfa ya Richmond iliyotokea katika uongozi wake na kuliingizia Taifa hasara ya mabilioni ya shilingi.Mpaka sasa hakuna kidhibitisho kuwa huyu mheshimiwa anahusika.
NO.10:MIZENGO KAYANZA PETER PINDA
NO.10:MIZENGO KAYANZA PETER PINDA
Huyu ni Waziri Mkuu Mteule.Alizaliwa Mkoani Rukwa ana elimu ya Chuo kikuu cha Dar es salaam,Ambapo alijiunga mwaka 1971 na kuhitimu mwaka 1974 kwa kupata shahada ya kwanza ya sheria (LLB).
Bw,Pinda ambaye ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mashariki,Kati ya Mwaka 1974 na Mwaka 1978 alikuwa akifanya kazi kama Mwanasheria katika Wizara ya Sheria kabla ya kwenda Ikulu Mwaka 1978 kuwa Ofisa Usalama wa Ikulu hadi mwaka 1982.
Kuanzia mwaka 1982 aliteuliwa kuwa Katibu Msaidizi wa Rais chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,na Mwaka 1996 hadi Mwaka 2000 alikuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri .
Waziri Mkuu Mteule,BwPinda kuanzia Mwaka 2000 hadi 2005 alikuwa Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mwaka 2006 hadi hadi anateuliwa kuwa Waziri Mkuu,aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,(TAMISEMI).
JENGA MAWAZO MAZURI,SAHAU YALIYOPITA,SONGA MBELE NA MAISHA.
Mara nyingi tumekuwa tukiumizwa sana kwa matukio yanayotokea katika Maisha Yetu ya kila siku na kuumizwa zaidi na wale wanaokuwa chanzo au wafanyaji wa matukio haya,Lakini hata sisi wenyewe tumekuwa tukijiumiza kila siku kwa kujifanyia mambo ambayo mwishowe huleta maumivu yanayobaki ndani ya mioyo yetu.
Jaribu kufikiria ni mara ngapi umekuwa ukiumia kwa kufikiria yale mabaya uliyofanya huko nyuma.Unaumia,unasononeka na kujikosesha raha pindi unapofikiria maovu uliyofanya huko nyuma na hii ni hatari sana,ukweli utabaki moyoni mwako,lakini chochote kilichokwisha tokea kimetokea na huwezi kubadili,Songa mbele na Maisha na kamwe usirudie kufanya kosa ulilokwisha kufanya,Muombe Mungu akupe uwezo na akili ya kufikiria mbele kwa yale yaliyo mazuri uliyopanga kuyafikiria uweze kufanikiwa maishani.Hakuna linaloshindikana kufanyika duniani hasa kama unamtumaini Mungu kwa kila jambo,ingawa kuna ugumu katika kufikia mafanikio ila bila kukata tamaa fanya ulilopanga kwa kujiamini.Sahau yaliopita songa mbele na Maisha,maisha ni mafupi mno,jipe raha mwenyewe na wacha kujikera na usiruhusu wengine kukukera.Jihadhari usije ukapata ugonjwa wa moyo na vidonda vya tumbo kwa kuwa na msongo wa mawazo.
2 comments:
Post a Comment