HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Saturday, August 28, 2010

IRAN YAZINDUA NDEGEVITA ISIYO NA RUBANI








Irani imezindua kile inachokisema ni ndegevita yake ya kwanza isiyo na rubani iliyotengenezwa nchini humo.
Rais Mahmoud Ahmadinejad alisema kwamba ndege hiyo inaweza kuwa ''mjumbe wa kifo'' lakini ujumbe wake muhimu ni wa kirafiki.Television ya Taifa ilionyesha ndege hiyo 'karrar'ikiruka.Ilisema ina uwezo wa kwenda kilometa 1,000 na kubeba mabomu yenye uwezo wa kilo 115 au makubwa zaidi.
Ndege hiyo ni ya kisasa katika orodha ya silaha mpya za kijeshi zilizozinduliwa nchini.
''...Ndege hii ni ujumbe wa heshima na ubinadamu na ukombozi wa binadamu,kabla ya kuwa mjumbe wa kifo kwa maadui wa binadamu...'' alisema Rais Mahmoud Ahmadinejad baada ya kuzindua karrar katika hafla iliyohuzuriwa na maafisa wa ulinzi.
''...Ujumbe muhimu ni urafiki...''aliongeza. ''tunapaswa kufanya juhudi za kuhakikisha silaha za maadui hazifanyi kazi kutokana na uwezo wetu kiulinzi''.
Uzinduzi huo umeendelea huku malalamiko ya yakiendelea dhidi ya mpango wa nyukilia wa nchi hiyo.
Nchi za magharibi zinaishuku Iran kwamba inajaribu kutengeneza bomu la nyukilia,ingawa serikali inasema mpango wake unalenga kukuza uwezo wake unalenga kukuza uwezo wa huduma ya nishati nchini humo.

No comments: