HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Monday, January 11, 2010

NYUMBA YAUNGUA KINONDONI SHAMBA

Nyumba yenye vyumba 6 iliyopo kinondoni shamba yanusurika kuteketea moto baada ya chumba cha uwani kuwaka moto uliosababishwa na mshumaa.Nyumba hiyo ilikuwa na vyumba 3 vya uwani vilikuwa vinajitegemea,mpangaji wa chumba kilichoungua ambaye ni raia wa malawi alishindwa kujieleza kwa polisi ambao walikuja kuchukua taarifa ya tukio hilo kwani alishikwa na pressure kwasababu yeye wakati chumba chake kinaungua (chumba cha uwani) alikuwa kibaruani.Mpangaji huyo alipoteza kila kitu kilichokuwepo ndani ya chumba hicho ambavyo viliteketea kwa moto,wasamaria wema walioitikia wito wa kusaidia kuzima moto walifanikiwa kuokoa godoro tu.

Wapangaji wenzake pia mbali na kunusurika kuunguliwa vitu vyao kutokana na moshi mzito uliokuwa umetanda nyumba nzima nikimaanisha hadi nyumba kubwa wasamaria wema hao hao walivunja milango na kuiba TV mbili,deck vyombo mbali mbali vya umeme begi lenye nguo na fedha kiasi cha 46,000 na vyombo vya chakula.
Mpangaji mmoja aliulizwa na polisi je unaweza kutuambia wewe umeibiwa nini akasema hawezi kujibu maana vitu vyangu vimevurugwavurugwa.

Wakati moto unapamba moto tulijaribu kuwasiliana na Fire lakini hawakuja.

Kinachoniuma ni watu walivyo na roho mbaya yaani jirani anaunguliwa na wewe unamwibia.Ndio maana mtaa huu wakikamata mwizi wanachinja.
Inashangaza mtaa nyumba iliyoungua ni nyumba ya 3 tu ambayo kijana Khaji Mkame aliyeuawa kinyama alikuwa anakaa lakini watu wamerudia kuiba tena kwenye tukio ambalo watu wana huzuni na hasira.

ONA JINSI KHAJI ALIVYOUAWA LAKINI WATU WANAIBA TU?
(BONYEZA HAPA CHINI)
EMAIL ME

No comments: