HIVI NDIVYO MTAANI KWETU WALIVYO,WATU WAMECHOSHWA NA MAJAMBAZI NA VIBAKA,HAWA JAMAA SIO KWAMBA HAWAFAAMIKI.HUYU JAMAA ALIYEVAA TSHIRT NYEKUNDU ANAITWA KHAJI MKAME NA UMRI WAKE KAMA MIAKA 24 HIVI,YEYE NI MZAWA WA KINONDONI SHABA NA AMEKULIA HAPA HAPA CHA AJABU WATU WAMEMUUA KIKATILI KAMA MTU AMBAYE HAFAHAMIKI.
KINACHOWAKERA WATU NI JINSI HUYU JAMAA ALIVYOKUWA HASIKII PINDI ALIPOKUWA AKIONYWA JUU YA TABIA YAKE YA WIZI,ALIKUWA AKITAKA KITU KWAKO KWA NGUVU,UKIONYESHA KUKATAA UTAONA CHA MOTO ATAHAKIKISHA AMEKUJERUHI VIBAYA HATA KAMA ANAKUFAHAMU (YAANI KAMA ALIKUWA NA PANGA AU KISU ATAKUJERUHI NACHO TU)
SASA USIKU WA KUAMKIA JUZI MNAMO SAA 9 USIKU WALIIBA FEDHA NA NGUO MAENEO HAYO HAYO YA KINONDONI SHAMBA,KWA BAHATI MBAYA KWAO ILIKUWA NI SIKU YAO YA 40.WALIKIMBIZWA NA KUPITA NYUMBANI,MIMI NILIPUUZIA NA KULALA.CHA AJABU ASUBUHI MAJIRA YA 12 ASUBUHI TULIAMSHWA TUKAANGALIE MAUJI YA KUTISHA YALIYOTOKEA MAENEO YA BIAFRA.
KUMBE HAWA JAMAA WALIPOKAMATWA WALIPEWA KIPIGO CHA KUTOSHA,KISHA WAKAAMBIWA TUTAWAPELEKA KIWANJANI BIAFRA ILI WANAWAKE WASIWAONEE HURUMA,WALIVYOFIKISHWA HUKU NDIPO KIPONDO CHA KUFA MTU KILIENDELEA.
INASEMEKANA NI BAHATI YAO MVUA ILIKUWA INANYESHA MAANA UNAVYOONA WAMEVESHWA MAPIRA WALIKUWA TAYARI WANATAKA KUBANIKWA LAKINI WALIPOMWAGIWA PETROL KIBERITI KILILOWA,WALIPOENDA KUCHUKUA KIBERITI KINGINE PETROL WALIYOKUWA WAMEMWAGIWA NAYO ILIKUWA IMEYEYUKA KUTOKANA MVUA KUBWA ILIYOKUWA IKINYESHA.
BONYEZA HAPA CHINI KUONA ZAIDI
http://zablonmacha.blogspot.com/
JE WALISTAHILI KUFANYIWA HAYA?,HATA KAMA WALIKUWA HATARI EMAIL ME
zabbyboy@gmail.com
JE WALISTAHILI KUFANYIWA HAYA?,HATA KAMA WALIKUWA HATARI EMAIL ME
zabbyboy@gmail.com
No comments:
Post a Comment