HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Friday, November 6, 2009

JE UNAUFAHAMU MWEZI








Mwezi wa dunia yetu ni mkubwa kushinda miezi mingine katika mfumo wa jua. Hakuna jina tofauti kuliko "mwezi" isipokuwa watu wametumia neno la Kilatini "luna" kwa ajili ya mwezi wakitaja mwezi wetu ili kuutofautihsa na miezi ya sayari nyingine.
Huwa tunaangalia uso wake upande mmoja tena uleule tu. Kwa hiyo kuna upande moja penye mchana na upande mwingine penye usiku wakati wowote. Sababu yake ni ya kwamba siku ya mwezi ni sawa na kipindi cha mwezi duniani. Mwezi unazunguka kwenye kipenyo chake katika muda wa siku 27.321 661 za dunia.
Uso wa mwezi unajaa mashimo ya kasoko yaliyosababishwa kwa kugongwa na meteoridi. Mwezi hauna angahewa inayozuia mapigo ya meteoridi ndogo au kupunguzu nguvu yao jinsi ilivyo duniani.


Mwezi wetu ni gimba la anga la kwanza ambako wanadamamu wamefika. Tarehe 21.07.1969 mwanaanga Mwamerika Neil Armstrong alikuwa mtu wa kwanza wa kukanyaga uso wa mwezi. Waamerika 11 walimfuata katika miaka hadi mwaka 1972. Baadaye safari za kwenda mwezi hazifanywa tena kutokana na gharama kubwa.


Hata kama Warusi na Waamerika walifisha mabendera yao mwezini wote hawadai mali kwenye mwezi. Katika mkataba wa kimataifa kuhusu anga wa nje Waamerika,Waingereza na Warusi walipatana ya kwamba mwezi utaangaliwa sawa na maeneo ya kimataifa ya bahari. Walipatana pia ya kwamba itakuwa marufuku kupeleka silaha kali kama kinyuklia angani. Mataifa mengi ya dunia yamejiunga na mkataba huo isipokuwa nchi mbalimbali za Afrika hawakutia sahihi kama vile Tanzania.
Lakini kuna watu binafsi wanaodai mali ya mwezi. Kwanza kuna familia ya Jürgens wanaoishi Westerkappeln (Ujerumani) walipewa hati ya kumiliki mwezi na mfalme wa Prussia Friederich II. tarehe 15.07. 1756 BK. Mfalme alitoa hati kama zawadi ya shukrani kwa huduma bora akiamuru ya kwamba Martin Jürgens atakuwa mwenye mwezi na haki hii itarithiwa na mtoto wa kwanza.
Bila shaka ilhali hakujua haki za mali za Mjerumani katika mwaka 1980 Mwamerika Dennis M. Hope alifika mbele ya msajili wa viwanda mjini San Francisco akidai mwezi ni wake. Kufuatana na sheria ya Marekani kiwanda ni mali ya mtu akiandikisha dai lake na katika muda wa miaka minane hakuna upingamizi dhidi ya dai lake. Kwa njia hii -iliyowahi kufaulu tayari wakati wa karne zilizopita Wazungu walipojipata Amerika ya Kaskazini (hakuna aliyepinga madai yao mbele ya msajili)- alipata hati ya kumiliki akijaribu kuuza sasa mwezi polepole.

No comments: