Michael Jackson (29 /10/1958 - 25/06/2009) alikuwa mwimbaji,mtunzi wa nyimbo,mtarishaji wa kurekodi,mwigizaji ,mfanyabiashara,mtunzi wa vitabu na kabaila kutoka nchini marekani. Alikuwa na vipaji vingi vya kisanii kama vile kuimba,kucheza na utunzi wa aina ya muziki wa pop. Katika miaka ya 1980 alivuma sana na albamu yake ya Thrille iliyovunja rekodi ya mauzo kwa kuuza nakala milioni 104.
Michael Jackson alianza kuonekana jukwaani akiwa na miaka 5 tu pamoja na kaka na dada zake.Alitokea katika familia ya wana muziki ya Jackson five, kuhusu maisha yake ya awali alisimulia mara kadhaa ya kwamba baba yake alimlazimisha mno kufanya mazoezi ya kucheza na uimbaji hivyo Michael alikosa utoto. Watazamaji wengi wamehisi ya kwamba matatizo ya kisaikolojia ya msanii yalikuwa na chanzo katika kipindi hiki.
Michael aliandika nyimbo nyingine maarufu ambazo ni 'Bad' na 'Black or White',huyu pia aliitwa mfalme wa pop duniani
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment