HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Tuesday, December 16, 2008

MFAHAMU ADOLF HILTER







Alizaliwa Austria mwaka 1889,alijiunga na shule ya Sekondari mwaka 1900 lakini hakufaulu hivyo alishindwa kuendelea na masomo. Alijaribu tena kurejea shuleni zamu hii katika shule ya uchoraji iliyojulikana kama Vienna Academy of Fire Art huko Vienna akafeli tena. Baada ya wazazi wake kufariki alikosa usaidizi wa familia akakaa kwa muda katika nyumba ya watu wasio na makazi.

Mnamo mwaka 1913 alihamia Munich katika jimbo la Bavaria (Ujerumani). Katika Agosti 1914 wakati wa mwanzo wa vita kuu ya kwanza ya Dunia alijitolea kwa jeshi la Bavaria na kutokana na kutokana na bidii na ukakamavu alipanda cheo na kuwa (praiveti). Mwisho wa vita mwaka 1918 alikuwa na cheo cha Koplo.

Baada ya vita alikosa kazi lakini aligundua kipaji chake cha kuhutubia watu, Akajiunga na siasa na kuingia katika chama kidogo cha Nazi alikopanda ngazi haraka. Hitler alivutwa sana na mfano wa Benito Mussolini kiongozi wa kifashisti wa Italia aliyefaulu mwaka mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano ya wafuasi wake kuelekea Roma.

Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumuiga Mussolini kwa kupindua Serikali ya Bavaria ikiwa ni kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin, lakini alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano lakini alitumikia miezi 9 tu. Na chama chake kupigwa marufuku.

Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa '' Mein Kampf '' (mapambano yangu) alijaribu kueleza imani na siasa zake. Humo alieleza pia itikadi yake ya Chuki dhidi ya Wayahudi. Hitler alipokuwa kijana aliwahi kusoma vitabu vya mwingereza Chamberlain aliyedai ya kwamba kuna mbari (rangi) mbali mbali kati ya watu wenye tabia na thamani tofauti sana. Katika itikadi hiyo mbari wa juu ni watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita ''Waaria'', wale ambao ni duni ni watu weusi. Vikundi vingine vipo katikati,juu au duni. Lakini watu wabaya kabisa katika itikadi hii ni wayahudi ambao ni wajanja,wakuu upande mmoja lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine. Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya waaria.

Hitler alifuata siasa ya kukusanya wajerumani wote katika Dola la Ujerumani. Mwaka 1938 alifaulu kuteka Austria na maeneo ya Wajerumani katika Uceki bila upingamizi wa kimataifa.

Aliposhambulia Poland mwaka 1939 tendo hili lilikuwa mwanzo wa vita kuu ya pili ya dunia kwa sababu Uingereza na Ufaransa walisimama imara kwa mikataba ya usaidizi na Poland.
Wakati wa vita Hitler alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi. Mwanzoni alifaulu hata dhidi ya ushauri wa majenerali wake, hasa dhidi wakati wa vita dhidi ya poland na Ufaransa. Lakini maazimio yake ya mwaka 1941 ya kushambulia Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya marekani yalikuwa mwanzo wa mwisho wake.

Nguvu ya uchumi ya Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote. Hitler alipoona vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa. Azimio la '' Usuluhisho wa mwisho wa swali ya kiyahudi '' lilichukuliwa mwisho wa 1941 na kutangaza mbele ya viongozi wachache Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee. Baadaye siasa ya kuwatendea Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo fulani,ilibadilishwa kulenga kwa Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake. Hadi mwisho wa vita wayahudi walikusanywa kote ulaya na kupelekwa kwa reli hadi makambi ya mauti.


MWISHO WA VITA NA KIFO CHAKE


Maafisa wa jeshi wa Ujerumani walipanga mara kadhaa kumuua Hitler. Tarehe 20 Julai 1944 alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberg lakini hakuuawa. Mwisho wa Vita Hitler alikaa Berlin hadi jeshi la Kirusi lilipoingia mjini humo. Tarehe 30 April alijiua kwa sumu pamoja na mpenzi wake Eva Braun (alimuoa masaa machache tu kabla ya kujiua) pamoja na mbwa wake mpenda '' Blondi '' Maiti zilichomwa kwa petroli lakini zilitambuliwa na warusi kutokana na meno yake

No comments: