Friday, January 20, 2012
HUYU NDIYE MGUNDUZI WA FACE BOOK
Mark Elliot Zuckerberg (amezaliwa 14 Mei, 1984) ni mjasiriamali Mmarekani anayejulikana kama mwanzilishi mwenza wa tovuti maarufu ya urafiki mtandao ya Facebook. Zuckerberg alianzilisha Facebook pamoja na wanafunzi wenzake Dustin Moskovitz, Eduardo Saverin, na Chris Hughes wakati wakihudhuria Chuo Kikuu cha Harvard. Zuckerberg ndiye Afisa Mkuu Mtendaji wa Facebook.[2] Amekuwa mada ya utata kuhusu asili ya biashara yake. [3]
Time magazine ilimworodhesha Zuckerberg kama moja wa Watu Mashuhuri Zaidi Duniani mwaka wa 2008. Aliorodheshwa katika kitengo cha Wanasayansi na Mamajuzi kwa mtandao wake ulionoga wa Facebook, na kuorodheshwa wa 52 kati ya watu 101 [4] Kufikia Januari 2010 Zuckerberg ndiye mfanyabiashara aliyejijenga mchanga zaidi mwenye thamani ya zaidi ya dola bilioni.
Maisha Yake ya AwaliZuckerberg alizaliwa White Plains, New York na kukulia Dobbs Ferry, New York. Alianza kuunda programu alipokuwa katikati shule ya kitengo cha kati. Zuckerberg alifurahia kuunda programu za kompyuta mapema, na hasa zana za mawasiliano na michezo. Kabla ya kuhudhuria Exeter Phillips Academy, Mark alienda shule ya Ardsley High School. "Katika shule ya upili, yeye alifaulu sana katika masomo ya Kale. Alihamishiwa Phillips Exeter Academy ambako alizama katika somo la Kilatini. [6][6]Pia aliunda programu ya kuwasaidia wafanyakazi katika ofisi ya baba yake kuwasiliana; akaunda toleo la mchezo wa Risk na programu ya kucheza muziki iitwayo Synapse iliyotumia wangafu kujifunza tabia za kusikiliza za watumiaji. Microsoft na AOL zilijaribu kununua Synapse na kumwajiri Zuckerberg, lakini aliamua badala yake kuenda Chuo Kikuu cha Harvard, ambapo alijiunga na Alpha Epsilon Pi , kikundi cha wanafunzi Wayahudi.[7]Chuoni, alijulikana kwa kukariri mistari kutoka mashairi ya kale kama vile The Iliad . [6]
Uanzilishi
Zuckerberg alivumbua Facebook katika chumba chake cha kulala cha Harvard mnamo Februari 4, 2004. Wazo la Facebook lilimjia kutoka siku zake za Phillips Academy Exeter ambapo, kama vyuo na shule nyingi, ilikuwa na mazoea ya siku nyingi ya kuchapisha kitabu cha kila mwaka chenye picha za wanafunzi wote, Kitivo na wafanyakazi inayojulikana kama "Facebook". Chuoni, Facebook ilianza tu kama "jambo la Harvard", mpaka Zuckerberg alipoamua kuieneza Facebook katika shule zingine na kuomba msaada kutoka kwa Dustin Moskovitz aliyekuwa wakiishi katika chumba kimoja chuoni. Kwanza walieneza hadi Stanford, Dartmouth, Columbia, Cornell na Yale, na kisha kwa shule nyingine zilizokuwa na mawasiliano ya kijamii na Harvard.
Facebook Platform
Mnamo May 24 2007, Zuckerberg ilivumbua Facebook Platform, jukwaa ya maendelezo kwa kujengea vipengele vya kirafiki ndani ya Facebook. Tangazo hili lilisababisha hamu kubwa katika jamii ya wanaotengeneza vipengele hivi. Katika wiki chache, vipengele vingi vilijengwa na baadhi zao tayari kutumika na mamilioni ya watumiaji. Hii leo, kuna zaidi ya watengenezaji 800,000 ulimwenguni wanaounda vipengele kwa kutumia Facebook Platform.
Mnamo Julai 23 2008, Zuckerberg alitangaza Facebook Connect, toleo la Facebook Platform kwa watumiaji.
Microsoft kuwekeza katika Facebook
Mnamo October 24 2007, Facebook Inc iliuza asilimia 1.6 ya hisa zake kwa Microsoft Corp kwa dola milioni 240, na kughairi maombi kutoa kwa kampuni inayoongoza katika huduma ya kutafuta katika mtandao Google Inc Hii ilionyesha kwamba Facebook ilikuwa na thamani ya dola bilioni 15 wakati wa mauzo. Programu ya kusasisha bidhaa ya michezo ya Xbox 360 ya Microsoft ilitolewa na pia kuboresha Facebook, Twitter na Last.fm [15]
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment