HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Sunday, October 3, 2010

BISHOP EDDIE LONG AZUSHIWA SKENDO!!!





Mtumishi wa Mungu mwenye uwezo mkubwa wa kuhubiri Neno la Mungu Bishop Eddie Long (na mpinzani mkubwa wa mahusiano ya kishoga) mambo yamemvurugukia (kama wenzake hawa) baada ya kushushiwa tuhuma nzito na wavulana wanne ambao walikuwa waumini wa kanisa lake. Wavulana hawa tayari wameshafungua kesi mahakamani na mwingine watano anategemea kufanya hivyo hivi karibuni.
Wavulana hawa wanadai kwamba Bishop alikuwa akiwalaghai kwa pesa, magari, vito vya thamani na safari za ndani na nje ya Marekani huku akijifanya kuwa kama "baba" kwao na baadaye kutumia nafasi hiyo kuanzisha uhusiano wa kingono.
Habari hizi zipo kila mahali huko Marekani na sasa kuna picha ambazo zinadaiwa kwamba Bishop alikuwa akiwatumia vijana hawa na "text messages" ambazo alikuwa akiwaomba pia wamtumie picha zao. Na kwa wanaopenda kuhukumu, tayari wameanza kupaza sauti wakidai ni lazima ajiuzulu wadhifa wake wa Uchungaji Mkuu wa kanisa kubwa la New Birth Missionary Baptist Church lenye waumini wapatao 25,000 wakiwemo watu mashuhuri mbalimbali.

No comments: