KAMANDA WA POLISI CELINA KALUBA ADHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILI.
KIBAKA mmoja ambaye hajafahamika jina lake wala makazi ameuawa kikatili na wananchi wenye hasira kali na kisha kuchomwa moto baada ya kufanya jaribio la kuvunja duka na kuiba bidhaa mbalimbali. Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi majira ya saa 10 alfajiri katika eneo la Mwenge Manispaa ya singida ambapo kibaka huyo alikuwa na wenzake watano. Kwa mujibu wa watu walioshuuhudia tukio hilo walisema kuwa vibaka hao wakiwa watano waliingia katika duka moja la Bw Daniel Miyanji na kuanza kuvunja mageti ya duka hilo na kuanza kutoa bidhaa mbalimbali zikiwemo bia na bidhaa nyingine. Akizunguma mmiliki wa duka hilo Daniel Miyanji alisema akiwa amelala usiku huo alisikia kelelel za mbwa wa jirani wakibweka mfululizo. "... Baada ya kusikia kelele za mbwa wa jirani muda mrefu niliamka na kuchungulia dirishani na kuona watu wakitoa vitu dukani kwetu, ndipo nilimwamsha kaka yangu na watu wengine juu ya tukio hilo ..." alisema . Miyanji alisema kuwa hapo ndipo waliungana na kuanza kuwakurupua vibaka hao ambapo katika kurupushani hizo walifanikiwa kumkamata kibaka aliyekuwa ndani ya duka akitoa mali kwa wenzake na kuanza kushambuliana. Alisema kuwa kibaka huyo alikuwa akiwatisha kwa kisu lakini kutokana na umoja wa wananchi waliofika kutoa msaada baada ya kupiga makelele walimzidi nguvu na hatimaye kuanza kumshambulia. "... Mimi na kaka yangu tualiza kuwafukuzia wale vibaka wengine ambao walikimbia na pesa ambazo hata hivyo idadi yake bado haijafahamika huku wananchi wakiendelea kumpa kibano kibaka huyo na hatimae kumchoma moto. Kamanda wa polisi Mkoani hapa Celina Kaluba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwaba polisi wanafanya uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwasaka vibaka wengiene waliohusika katika tuko hilo. Hata hivyo wananchi wa maeneo ya jirani wamesema kuwa hiyo ni mara ya tatu kwa duka hilo kuvamiwa na vibaka na kisha mali kuchuliwa ambapo mwenye duka hilo akiamka asubuhi anakuta duka jeupe na hivyo kumpunguzia nguvu kazi ya kujiletea maendeleo yake pamoja na familia yake. "... Jamani sisi tumechoshwa na hawa wezi kila mara wanamwibia huyo kijana wa hili duka hebu angalieni mali yote imetolewa nje na kama sio kushtuka si angekuta hamna kitu, tunasema tukikamata kibaka safari hii aaangalie mfano wa huyu mwenzao hatuna msaliamtume, polisi watakuja kuchukua majivu tu..." Alissisistiza mama mmoja jirani na eneo hilo la tukio
No comments:
Post a Comment