HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Thursday, December 18, 2008

JE UMEWAHI KUMSIKIA MAMA TERESA WA KOLKATA JINSI ALIVYOKUWA NA MOYO WA AJABU WA KUSAIDIA WATU MASKINI NA WENYE UHITAJI?, SOMA HISTORIA YA MAISHA YAKE


Mama Teresa wa Kolkata (26 Agosti 1910 - 05 Septemba 1997) alikuwa ni mtawa wa Kanisa katoliki aliyejulikana Kimataifa hasa kutokana na huduma yake kwa watu maskini katika mji wa Kolkata (UHINDI) iliyompatia tuzo ya Nobel ya Amani.
Alizaliwa tarehe 26 Agosti 1910 mjini Skopje katika familia ya Waalbania akaitwa Agnes Gonxha Bojaxhiu. Alipofika umri wa miaka 18 alijiunga na Shirika la Masista wa Loreto huko Ireland na mwaka 1929 alitumwa Uhindi akafundishe kwenye shule ya Masista mjini Kolkota alipoendelea kuwa mkuu wa shule.
Aliguswa sana na hali ya umaskini nje ya shule akajisikia wito wa kuwasaidia na kuishi pamoja nao. Kwa kibali cha wakubwa wa shirika lake na wa kanisa mwaka 1948 alitoka jumuiya na Loreto akaanzisha maisha duni kati ya wakazi wa mitaa ya vibanda.
Alianzisha shule lakini baada ya muda alitambua umuhimu wa kuzingatia zaidi hali ya watu waliokuwa wagonjwa na kufa katika mitaa ya vibanda. Mwaka 1950 alianzisha shirika la Masista Wamisionari wa Upendo ambalo mwanzoni lilikuwa jumuiya ndogo ya masista 12 tu. Kati ya kazi zao za kwanza ilikuwa ni nyumba kwa watu mahututi, Masista waliwakusanya watu barabarani na kuwapeleka katika nyumba walipopata dawa,chakula na usaidizi.
Shirika lilikuwa haraka sana na mpaka leo kuna Masista zaidi ya 4,000 kwa jumla katika matawi mengi kote duniani. Kazi wanazoendelea kuzifanya ni kuendesha nyumba kwa watoto Yatima, wagonjwa wa Ukimwi, Wenye Ukoma, Walemavu, Walevi na kila aina ya matatizo maishani.

Mwaka 1979 alipewa tuzo ya Nobel ya Amani
Mama Teresa aliaga dunia mwaka 1997 akatangazwa na Papa Yohane Paulo II, kuwa ni Mwenye Heri. Baada ya kifo chake maandishi yake yaliyotolewa yalifichua siri ya maisha yake ya ndani, yaani kupita kwa karibu miaka 50 mfulululizo katika hali ngumu inayoitwa usiku wa roho bila ya ya kuweza kumzuia atabasamu muda wote

No comments: