HIVI SASA NI SAA

TAREHE

Wednesday, August 25, 2010

WANASAYANSI WASEMAVYO KUHUSU WATU KUISHI ZAIDI YA MIAKA 100






Wengi wetu tunapenda kuishi maisha marefu kwa kadri iwezekanavyo. Maendeleo ya sayansi na teknolojia na hasa maendeleo makubwa katika taaluma ya tiba na kuimarika kwa hali ya maisha kwa ujumla hasa katika nchi zilizoendelea kumeleta uwezekano wa watu kuishi miaka 100 na hata zaidi.

Katika utafiti mpya kabisa, wanasayansi, wanaonya kwamba watu wachache wanaoishi miaka 100 na hata zaidi wanafanya hivyo kutokana na sababu za kibayolojia/kimaumbile. Watu hawa wana chembechembe za uhai maalumu ambazo zinawasaidia kutopatwa na magonjwa ya kawaida yanayosababisha vifo kwa wazee.

Baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa chembechmbe za uhai za watu 1000 wenye umri wa miaka 100 na zaidi, wanasayansi sasa wanaweza kutabiri kwa usahihi wa asilimia 73 uwezekano wa mtu kuishi hadi kufikisha miaka 100 na zaidi.

Kama una wazazi, babu na bibi, wajomba, mashangazi, na ndugu wengine wa karibu ambao waliishi hadi miaka 100 au zaidi basi kuna uwezekano mkubwa kwamba familia au ukoo wenu umeshinda bahati nasibu ya kimaumbile ya kuishi maisha marefu.

Pamoja na hayo, wanasayansi wanaonya kwamba hata kwa watu ambao wamejaliwa kurithi chembechembe hizi nzuri za urithi, bado wanahitajiwa kuishi maisha yenye kuzingatia afya njema mf. kufanya mazoezi mara kwa mara, kutokunywa pombe kupindukia, kutovuta sigara na kutonenepa kupindukia

No comments: